NCHI YA MIGOMO

NCHI YA MIGOMO
Katiba ya Kenya inamruhusu mtu yeyote kuandamana au kufanya mgomo ili kuelezea malalamishi yake au kutoa shinikizo. Kinachoshangaza ni kwamba nchini Kenya migomo imekuwa ni jambo la kawaida na katika kila sekta ya wafanikazi, tumeshuudia mgomo.Tukianza na walimu, wauguzi na madaktari, wafanyikazi wa vyuo pamoja na wanafunzi na kila mfanyikazi amewahi kushiriki mgomo kupitia maandamano au hata mgomo baridi. Swali ni je, mgomo unapotokea hasa wa wafanyikazi wa umma, ni nani huathirika zaidi?

Walimu wamekuwa na migomo tangu nizaliwe wakipigania ongezeko la mishahara.Walimu hao wanaposusia kazi wakilalamikia malipo duni, wanawaacha wanafunzi ambao ni watoto wa wakenya wenzao masikini bila kufunzwa.Wakubwa serikalini wanaoshinikizwa hawana cha kupoteza kwa sababu watoto wao husomea shule za kibinafsi na hata nje ya nchi. Kwa hivyo hapa, masikini anamnyima masikini mwenzake elimu.
Kwa muda mrefu, watu wengi walimheshimu daktari na muuguzi na watu wengi walitamani sana kuingia katika taaluma hii. Hata hivyo, kwa kugatuzwa kwa huduma za afya katika kaunti mbalimbali imefanya tushuhudie migomo hatika sekta hii muhimu.

Hawa hulalamikia hasa mazingira duni ya kazi na athari za mgomo wao tena huonekana kwa mkenya masikini. Wakuu serikalini hutibiwa katika hospitali ya kibinafsi au nchi nyingine zenye huduma bora za kiafya kema vile Misri, Marekani au Wingereza.

Mkenya masikini hapati usaidizi wa matibabu anapohitajika na tumeshuhudia vifo ya watu wengi hospitalini na hata kina mama kujifungua bila usaidizi wa muuguzi. Hakuna hata anayeshughulikia waathiriwa wa mkasa, kisa na sababu wauguzi wamegoma wakitaka ongezeko la mishahara.Ama kweli masikini ana taabu.
Migomo na maandamano pia huchangia utovu wa usalama kwa wanaoshiriki pamoja na wasioshiriki. Katika mandamani mengi, tumeona watu wakijeruhiwa na wengine hata kupoteza maisha yao.Septemba mwaka wa 2012, walimu waliokuwa kwenye mandamano walimvamia, kumjeruhi na kumvua nguo hadharani mwalimu mwenzao kwa kutoshirikiana nao katika maandamano. Maandamano katika kaunti ya Narok yalipelekea kifo na majeruhi na yalotokea wakati wa maandamano. Hii ni kwa sababu wakenya hawatambui chochote kama maandamano ya amani na maandamano bila vitoamachozi sio maandamano. Nambie hawa wanaojeruhiwa na hata kuangamia ni nani kama sio wakenya wa kawaida.

Kauli yangu ni kwamba wakati wa maandamano, wanaoathirika sio wanaogomewa bali ni wanaogoma wenyewe. Walimu wakigoma, ni watoto wao hawasomi. Wauguzi wakisusia kazi, ni watoto, mabibi, ndugu na dada zao masikini hukosa huduma za kimatibabu. Ghasia zikitokea, bado ni wenyewe tu huumia.
Nchi ya migomo haiwezi kuendelea kwa sababu maandamano na migomo huhujumu nchi kiuchumi kiusalama na maisha ya masikini huendelea kuwa magumu zaidi. Hii ni nchi ya ubepari ambapo masikini huzidi  kuwa masikini huku tajiri akitajirika zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

A UNIVERSITY OF OUR TIME

AFRICAN INDEPENDENCE POLITICAL PARTIES THAT RULE TO DATE.

REIMBURSEMENT IN CAMPUS LEADERSHIP